Boresheni hali ya wafanyakazi :Amnesty

Image caption Maandalizi ya kombe la Dunia

Shirika la kupigania haki za binadamu la Amnesty International ,linasema Qatar inalazimika kuboresha hali ya wafanyakazi wahamiaji wakati huu nchi hiyo inapoendelea na maandalizi ya kombe la dunia la mwaka 2022.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wafanyikazi wa kigeni ndio wanaotumika kujenga viwanja Qatar

Amnesty wanasema Qatar imepiga hatua kidogo sana kutekeleza ahadi nyingi walizozitoa mwaka jana, kwani wafanyakazi bado wanahitaji ruhusa kutoka kwa waajiri wao ,kubadili ajira au kuondoka nchini humo,mabadiliko ya malipo kwa wafanyakazi yanafanyika taratibu mno wakati ni jambo la muhimu mno.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya wafanyikazi wanasemekana kuishi katika mazingira duni

Hata hivyo Serikali ya Qatar inasema mabadiliko makubwa yanakuja ifikapo mwishoni mwa mwaka huu,japo kuwa Amnesty inaitaka FIFA , kuishinikiza Qatar kuongeza kasi katika kuleta mabadiliko.