Ireland yaamua kuhusu ndoa za jinsia moja

Image caption Kura ya maoni kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja Ireland

Shughuli ya upigaji kura inaendelea huko Ireland katika kura ya maoni ya kubadilisha katiba ili kuruhusu ndoa za mapenzi ya jinsia moja.

Iwapo mabadiliko hayo yataidhinishwa,Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja kwa wingi wa kura.

Matokeo ya kura hiyo yanatarajiwa jumamosi mchana.