Wapiganaji wa IS waelekea Baghdad

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Isis

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wanaimarisha maeneo waliyoyateka nchini Syria na Iraq.

Wameripoti kuliteka eneo la mpakani la mwisho lililokuwa likidhibitiwa na serikali.

Nchini Iraq wanaonekana kuvunja ulinzi wa serikali nje ya Habbaniyah,ambapo wapiganaji wa kishia wanakongamana ili kutekeleza mashambulizi.

Wapiganaji hao wa jihadi wanaelekea mashariki karibu na mji wa Baghdad.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption wapigani wa shia nchini iraq

Muungano wa waasi wa Syria wakati huohuo unasemekana kuiteka hospitali moja ambapo karibu wanajeshi 150 wazungukwa kwa takriban mwezi mmoja sasa.

Runinga ya serikali ya Syria inasema kuwa wanajeshi hao walisalimu amri.