Wanaopinga ndoa za jinsia moja wasalimu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiga kura wa Ireland

Huku kura zikiendelea kuhesabiwa baada ya kura ya maoni nchini Ireland kuhusu uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja,kiongozi mmoja anayeongoza kampeni za kupinga ndoa hizo amekubali kushindwa.

David Quinn,kiongozi wa taasii ya iona inayokuza dini katika jamii ,aliwapongeza wanaotaka sheria kubadilishwa.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa baadaye jioni.

Iwapo mabadiliko hayo yataidhinishwa ,Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuruhusu ndoa za jinsia moja kupitia wingi wa kura.