Zaidi ya watu 40 wauawa Mexico

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi nchini Mexico

Takriban watu 43 wameuawa wakati wa ufyatulianaji wa risasi katika jimbo la Michoacan nchini mexico kati ya vikosi vya usalama na genge moja lenye silaha.

Mapigano hayo yalianza wakati magari ya polisi yalipofyatuliwa risasi kwenye barabara moja kuu katika kijiji kilicho karibu na mpaka na jimbo la Jalisco.

Moja ya megenge hatari zaidi ya madawa ya kulevya, liko eneo hilo na limekuwa likipigana vita vigumu katika jimbo la Michoacan kwa miaka mingi.

Maafisa kutoka kwa idara za usalama wanaelekelea eneo hilo kufanya uchunguzi.