Salva Kiir:Vikwazo vitachochea vita

Image caption Salva Kiir

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa vikwazo vya kimataifa vitachochoea zaidi vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Muungano wa Afrika na shirila la maendeleo la nchi za kusini mwa afrika IGAD wametishia vikwazo huku kukiwa na shutuma kuwa rais Kiir na hasimu wake Riek Machar wameshindwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya nusu ya watu wanahitaji msaada huku wengine milioni 2.5 wakikabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula.