Mbunge auawa Somalia

Haki miliki ya picha
Image caption Somalia

Watu waliojihami na silaha nchini Somalia wamemuua kwa kumpiga risasi mbunge mmoja na kumjeruhi vibaya mwingine kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishi.

Maaafisa wa usalama walisema kuwa Yusuf Dirir alikuwa ndani ya gari na mbunge mwingine wakati watu waliokuwa na silaha ndani ya gari jingine walipowamiminia risasi.

Kundi la wanamgambo la Al-Shabaab limetekeleza mauaji ya wabunge wengi nchini Somalia wakati wanapojaribu kuipindua serikali ya Somalia inayotambuliwa kimataifa.