Wanaharakati waingia Korea Kaskazini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Korea Kaskazini

Kundi la wanaharaklati wanawake wamevuka eneo lenye ulinzi mkali la mpaka kati ya Korea Kaskazini na Kusini katika jitihada za keleta mapatano.

Wanawake hao 30 ambao wamekaa siku kadha nchini Korea Kaskazini walitumia basi baada ya ombi lao la kutaka kuingia kwa miguu kukataliwa.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wanaharakati hao walipinga shutuma kuhusu safari yao nchini Korea Kaskazini na kuitaja hatua hiyo kuwa ya kihistoria.

Kiongozi wao alisema a kuwa wanawake hao wana lengo la kuonyesha mateso ambayo tofauti kati ya nchi hizo zimeleta.