Uchaguzi Hispania ushindani mkubwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiga kura Hispania

Dalili za awali katika uchaguzi nchini Hispania zinaonyesha huenda vyama vipya vikapata ushindi zaidi ya vile ambavyo vimekuwepo kwa miongo kadhaa.

Kuelekea mwisho wa uchaguzi huo matokeo yanaonyesha dalili za vyama hivyo vipya kuelekea ushindi kutokana na utafiti wa awali.

Hata hivyo vyama vya mlengo wa kushoto Podemos na vile vya mlengo wa kati kulia Ciudadanos vimeonekana kupata ushindi katika maeneo mengi.

Ajenda inayobebwa na waendesha kampeni wengi katika uchaguzi huo ni kutokomeza rushwa, majimbo ya Madrid na Barcelona katika uchaguzi huo ndiyo yameonekana kuwa kikwazo kwa wagombea wengi.