Polisi aondolewa mashtaka Marekani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waandamanaji katika mji wa Cleveland

Utawala katika jimbo la Ohio nchini marekani umetoa wito wa kutaka kuwepo utulivu baada ya polisi mmoja kuondolewa mashtaka yanayohusiana na kesi ambapo akiwaua wapenzi wawili mjini Cleveland miaka mitatu iliyopita.

Kumekuwa na maandamano yenye hasira lakini yaliyotulia mjini humo baada ya Michael Brelo kuondolewa mashtaka ya kuwaua Timothy Russel na Malissa Williams.

Polisi huyo alifyatua jumla ya risasi 15 kupitia kwa kioo cha mbele cha gari lao baada ya jumla ya magari 62 ya polisi kulifuata kwa kasi kimokosa gari lao.