Israeli:waziri wa zamani Olmert ahukumiwa

Haki miliki ya picha AFP Getty Images
Image caption Mahakama mjini Jerusalem imemhukumu waziri wa zamani wa Israeli Ehud Olmnert miezi 8 jela kutokana na mashtaka ya ufisadi.

Mahakama mjini Jerusalem imemhukumu waziri wa zamani wa Israeli Ehud Olmert miezi 8 jela kutokana na mashtaka ya ufisadi.

Alipatikana na hatia mwezi machi kwa kupokea pesa kinyume cha sheria kutoka kwa mfanyibiashara mmoja kutoka Marekani miaka ya 90.

Mwaka uliopita Olmert alihukumiwa miaka 6 jela kwa makosa ya ufisadi.

Anabaki kuwa huru ahadi pale atakapo kata rufaa kwa hukumu hizo zote.

Bwana Olmert alilazimishwa kujiuzulu miaka sita iliyopita na kutoa nafasi ya kuchaguliwa kwa waziri mkuu mweye msimao mkali Benjamin Netanyahu.