Makaburi 140 yapatikana Malaysia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makaburi 140 yapatikana Malaysia

Polisi nchini Malaysia wanasema kuwa wamepata karibu makaburi 140 na kile wanaamini kuwa ni kambi 28 haramu za kuwasafirisha watu kimagendo karibu na mpaka na Thailand.

Mkuu wa polisi nchini Malaysia Khalid Abu Bakar, anasema wanaamini kuwa makaburi mengine yanazaidi ya maiti moja.

Aidha makaburi hayo yalitumiwa kuzika wahamiaji ambao walikufa wakiwa kizuizini.

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Ugunduzi kama huo ulifanyika nchini Thailand

Ugunduzi kama huo ulifanyika nchini Thailand yapata mwezi mmoja uliopita na kutibua operesheni kali dhidi ya walanguzi wa binadamu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mkuu wa polisi nchini Malaysia Khalid Abu Bakar, anasema wanaamini makaburi mengine yako na zaidi ya maiti moja

Oparesheni hiyo iliyoendeshwa na jeshi la wanamaji na polisi wa Thailand iliwaacha maelfu ya watu wakiwa wametelekezwa baharini ,na ikalazimu mashirika ya kupigania haki ya kibinadamu na wakimbizi kuingilia kati ilikuzishinikiza serikali za mataifa husika kuwaruhusu wahamiaji waliokuwa kwenye mashua hizo za wakimbizi kuweka nanga katika bandari zao.

Operesheni hiyo ilikuwa inawalenga walanguzi wa watu wa jamii ya waislamu wa Rohingya kutoka Myanmar na Bangladesh.

Waziri wa masuala ya ndani wa Malaysia aliviambia vyombo vya habari kuwa ameshangazwa kugundua kuwa huenda kambi hizo zimekuwa eneo hilo kwa miaka mitano.