Nitabaki Real Madrid: Bale

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kiungo cha klabu ya Real Madrid Gareth Bale amesema atasalia katika timu hiyo.

Kiungo wa Real Madrid Gareth Bale ameelezea matarajio yake ya kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo msimu ujao, japokuwa kumekuwepo na tuhuma nyingi kutoka kwa mashabiki wa Madrid na baadhi ya vyombo vya habari nchini Hispania kutoridhishwa na kiwango cha mwanandinga huyo ikilinganishwa na pesa zilizotumika kumnunua.

Bale ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter huku timu hiyo ikitangaza kuachana na kocha wake Carlo Ancelotti. "nitajituma katika kipindi hiki ambacho msimu umeisha na kutazama mbele juu ya kurejea tena kwenye msimu ujao nikiwa na nguvu pamoja na Real Madrid" aliandika Bale. Mchezaji huyo alijiunga na miamba hiyo ya soka nchini Hispania mwaka 2013 akitokea Tottenham na amekuwa akihusishwa kurejea tena katika ligi ya England.