Mawaziri 4 kenya kizimbani kwa ufisadi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Tume ya maadili na kupambana na Ufisadi nchini Kenya EACC imewasilisha hati za kesi za Mawaziri wanne kwa mwendesha mashtaka mkuu wa Umma nchini humo.

Ofisi ya Mkuu huyo wa mashtaka nchini kenya, imebainisha kwamba EACC imependekeza kushitakiwa kwa Mawaziri wawili ambao uchunguzi umewakuta na makosa ya ufisadi na ukiukaji wa maadili katika sekta ya Umma

Mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya Dr. Keriako Tobiko amethibitisha kupokelewa kwa ripoti ya hali ya rushwa kutoka katika kitengo cha maadili cha kupambana na rushwa .

Na amebainisha kwamba ripoti hiyo imeweka bayana kuwa viashiria vya kushtakiwa kwa mawaziri wawili wa serikali ya Kenya viko wazi ambao ni Waziri wa usafirishaji ,Michael Kamau na mweziwe wa Wizara ya kazi Kazungu Kambi ,kwa tuhuma za kutumia ofisi zao vibaya.

Michael Kamau yeye anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha kwa kubadili michoro ya barabra ambayo tayari ilishafanyiwa uhakiki na watalaalam wa ujenzi .Naye waziri wa kazi ,Kazungu Kambi ameshutumiwa kila wakati kufanya uteuzi wa maafisa wawili kufanya kazi katika bodi za mashirika ya mifuko ya hifadhi za jamii .

Hata hivyo wale wote wanaoshutumiwa kwa ubadhirifu , rushwa na ukiukwaji haki za binaadamu huwa hawatajwi katika orodha za mafisadi wakati wengine orodha za majina yao tayari hayaonekani tena katika orodha hizo.