AfDB kupata rais mpya kumrithi Kaberuka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Benki ya maendeleo Afrika, Donald Kaberuka

Benki ya Maendeleo ya Afrika inaendesha shughuli zake chini ya uongozi wa rais, ambaye anafanya kazi kama mwakilishi halali wa Benki, mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na mnadhimu wa Benki hiyo. Rais anaendesha shughuli za sasa za Benki, chini ya maelekezo ya Bodi ya Wakurugenzi. Rais huchaguliwa na Bodi ya Magavana na anahudumu kwa miaka mitano. Pia anaweza kurudia kipindi kimoja tu cha miaka mitano mingine.

Rais wa sasa wa AfDB, Dr. Donald Kaberuka, raia wa Rwanda, alichaguliwa mwezi Julai 2005,na alianza awamu yake ya kwanza Septemba Mosi 2005. Kufuatia kuchaguliwa kwake tena mwezi Mei 2010, alianza kipindi chake cha pili cha miaka mitano mingine Septemba Mosi 2010. Kwa mujibu wa taratibu za uongozi katika Benki hiyo, Bodi ya Magavana inalazimika kumchagua mtu mwingine kuchukua nafasi hiyo

Wanaowania kushika nafasi hiyo ni:

Birima Sidibe, Mali Birama Sidibe ni mhandisi ambaye amejikita katika utaalam kilimo umwagiliaji. Kwa zaidi ya miaka thelathini, alikuwa akifanya kazi katika sekta ya maendeleo. Alifanya kazi na Benki ya Maendeleo ya Afrika tangu mwaka 1983-2006. Birama Sidibé pia alifanya kazi katika benki ya Maendeleo ya kiislamu, mjini Nairobi na kwa ajili ya shirika la River Senegal.

Haki miliki ya picha
Image caption Benki ya Maendeleo ya Afrika

Jalloul Ayed, Tunisia Jelloul Ayed ni mfanyakazi wa benki mwenye mafanikio nchini mwake na ana umri wa miaka 64. Yeye pia anajulikana kwa kuendesha harambee ya kuchangisha fedha zilizotolewa katika soko la Ulaya kwa ajili ya kampuni za Tunisia na Morocco. Mwaka 2011, akiwa waziri wa fedha wa mpito wa serikali baada ya kuanguka kwa Serikali ya aliyekuwa rais wa Tunisia Ben Ali, aliwahi kuwasilisha programu ya maendeleo ya kijami na kiuchumi katika mkutano mkuu wa G8. Bedourma Kordje, Chad, Ni waziri wa fedha nchini Chad sasa ivi, huyu mhandisi wa mawasiliano ya simu kwa miaka 29 ameitumikia benki ya maendeleo Afrika kabla ya kurudi nchini kwake na kuwa waziri wa fedha mwaka 2012. Rais Idriss Deby ameahidi kushawishi wanachama wa jumuiya ya afrika ya kati kwa ajili ya uchaguzi wa benki ya maendeleo ya Afrika AfDB.

Cristina Duarte, Sura Verde Ni mgombea mwanamke pekee kwa nafasi hii, lakini si kwa sababu yeye ni mwanamke, bali Anataka aangaliwe kwa uwezo wake wa kazi pia na si jinsia yake. Amelirudia mara kadhaa hilo na pengine ni sahihi. Amekuwa waziri wa fedha wa nchi yake tangu mwaka 2006. Anasifa kubwa ya kufanya mageuzi na kunyanyua uchumi wa nchi yake. Amefanya kazi pia na mashirika tofauti ya kimataifa ya kuleta maendeleo. Adesina Akinwumi, Nigeria Ni waziri wa sasa wa Kilimo na Maendeleo ya vijijini, Nigeria. Ana miaka 55 na amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA). Elimu yake ni shahada ya juu ya uzamivu katika uchumi wa Kilimo.Jarida liitwalo Forbes lilimtunuku jina la mwafrika wa mwaka 2013 kutokana na mageuzi yake katika sekta ya Kilimo.

Image caption Wanaowania Urais wa Benki ya maendeleo Afrika

Sufian Ahmed, Ethiopia Waziri huyu wa fedha na maendeleo ya kiuchumi mwenye umri wa miaka 57 anataka kutumia matokeo mazuri ya kiuchumi ya nchi yake kama mtaji kwa ajili ya kazi anayo iomba. Anasifika kwa kiasi kikubwa sana kwa kuwa na mchango mkubwa wa kiuchumi nchini mwake. Kamishna huyu wa zamani wa Mamlaka ya Forodha Ethiopia anajichukulia kama mwanamatumaini wa kiafrika. Pia elimu yake yote ameipatia nchini mwake.

Samura Kamara, Sierra Leone Ni mfanyakazi wa zamani wa shirika la fedha duniani, IMF na sasa ni waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa pia ni mwanamchumi mzoefu. Hiyo ni sababu kuu ya Rais Ernest Bay Koroma ametaka awe mjumbe wa serikali yake. Yeye awali alikuwa waziri wa Fedha. Ushirikiano wa Afrika ni kati ya mada kuu ya kampeni zake.

Thomas Sakala, Zimbabwe SADC imemchagua Raia wa Zimbabwe huyu kuwa mgombea wa kanda ya kusini mwa Afrika. Alistaafu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika mwaka jana tu na hadhi yake hiyo inaweza kuwa msaada mkubwa kwenye kinyang'anyiro hicho. Alifanya kazi na serikali nyingi za Afrika katika programu mbalimbali. Yeye anapigia upatu maendeleo ya miundombinu miongoni mwa masuala mengine.