Wakatoliki wajiondoa kwenye uchaguzi Burundi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Burundi:WaKatoliki wajiondoa kwenye uchaguzi

Kanisa Katoliki nchini Burundi limejiondoa katika mchakato mzima wa uchunguzi na uongozi wa aina yoyote katika uchaguzi huo.

Uamuzi huo umekuja wakati ikisalia wiki moja tu uchaguzi wa wabunge na madiwani ufanyike nchini humo

Kanisa katoliki ni kiungo muhimu katika suala la amani na demokrasia nchini Burundi tokea kuanzishwa mazungumzo ya amani ya Arusha mnamo miaka ya tisini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption EU inasema kuwa uamuzi wao umeafikiwa kwa sababu ya sheria kali dhidi ya vyombo vya habari na waandamanaji

Haya yamearifiwa wakati maandamano dhidi muhula wa tatu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza yanaendelea kufanyika katika mitaa kadhaa ya mji mkuu Bujumbura kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Wakati huohuo, Jumuia ya bara ulaya imesimamisha ujumbe wake uliokuwa usimamie uchaguzi mkuu nchini Burundi.

EU inasema kuwa uamuzi huo umeafikiwa kwa sababu ya sheria kali dhidi ya vyombo vya habari, matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji, na mazingara mabaya ya vitisho kwa vyama vya upinzani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Nkurunziza anapania kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu

Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki wakati wa ghasia za maandamano,

tangu rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mwezi uliopita kuwa anapania kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu, kinyume na katiba ya Burundi.

Uchaguzi wa urais umepangiwa kufanyika Juni tarehe tano, huku ule wa urais ukiwa mwishoni mwa mwezi huo wa Juni.