Nchi 17 kujadili tatizo la wahamiaji

Image caption Wahamiaji haramu

Viongozi wa nchi 17 Ulimwenguni wanakutana mjini Bangkok nchini Thailand kutafuta mbinu bora za kukabiliana na tatizo linalozidi kuongezeka la wahamiaji haramu wanaotoka Myanmar na Bangladesh maeneo ambayo nchi zake zinaoongoza kwa kuwa na idaidi kubwa ya wahamiaji.

Miezi kadhaa iliyopita maelfu ya wahamiaji haramu walitua katika pwani ya mwambao wa bahari ya Indonesia,Malaysia na Thailand. Hata hivyo wengi wa wahamiaji hao walijikuta wakizama baharini huko nchini Thailand mapema mwezi huu.

Awali Myanmar ilikataa mwaliko huo lakini safari hii imeamua kutuma ujumbe kushiriki mkutano huo. Wahamiaji walio wengi ni wa madhehebu ya Rohingya wanaokimbia mateso na umasikini katika nchi zao ikiwemo Myanmar na Bangladeshi na