Gill asusia wadhfa wa FIFA

Image caption Gill asusia wadhfa wa FIfa

Naibu mwenyekiti wa shirikisho la soka la Uingereza David Gill amekataa kuhudumu kama mwanakamati wa kamati kuu ya FIFA Sepp Blatter akiwa Rais.

Gill ambaye amechaguliwa jana anasema kuwa ''jina lake hadhi yake na jina baya la fifa haviambatani''

''Kwa hakika sioni nini kipya kitatokea baada ya kuchaguliwa upya kwa Sepp Blatter''

Gill ambaye aliwahi hudumu kama mkurugenzi mkuu wa timu ya Manchester United anapaswa kuhudumu kama mmoja wa makamu wa rais wa FIFA akiwakilisha Uingereza.

''Siamini kuwa Blatter alichaguliwa kwa njia ya haki na ukweli kwa hivyo mimi simtambui kama rais wa FIFA'' alisema Gill

''Hata hivyo nitaendelea kuhudumu katika wadhfa wangu katika shirikisho la soka barani ulaya na vilevile katika shirikisho la soka la Uingereza FA''.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gill, 57, alichaguliwa miezi 4 iliyopita kwa kipindi cha miaka 4.

Gill, 57, alichaguliwa miezi 4 iliyopita kwa kipindi cha miaka 4.

Sasa haijulikani iwapo atachaguliwa mtu mwengine ilikuchukua pahala pake ilikuipa uingereza usemi katika soka ya Ulaya na duniani.

Blatter amechaguliwa jana usiku kama rais kwa muhula wa tano.

Blatter alimshinda mwanamfalme Ali bin al-Hussein wa Jordan katika uchaguzi ambao ulikumbwa na kashfa ya ufisadi na ulaji rushwa.