Polisi wanaua watu 2 kila siku Marekani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Takwimu zilizokusanywa na gazeti la Washington Post zinaonyesha kuwa Polisi wanawaua watu wawili kila siku.

Takwimu zilizokusanywa na gazeti la Washington Post zinaonyesha kuwa Polisi wanawaua watu wawili kila siku.

Takwimu hiyo inaonyesha kuwa idadi ya watu wanaouawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi nchini Marekani ni ya juu kuliko inavyodhaniwa

Gazeti hilo linasema kuwa wakati wa kipindi cha miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu takriban watu 385 waliuawa ikiwa ni zaidi ya watu wawili kila siku.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa idadi ya watu weusi ilikuwa ni ya juu mno hasa wale ambao hawakuwa na silaha yeyote.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Takwimu hiyo inaonesha kuwa tangu mwaka wa 2008 watu 400 wanauawa kila mwaka na polisi.

Marekani imeshuhudia visa kadha ambapo watu weusi wanauawa na polisi wazungu .

Visa hivyo vimetibua maandamano makubwa huku wanaharakati wa kupigania haki za binadamu wakisema polisi wanawalenga watu weusi.

Takwimu hiyo inaonesha kuwa tangu mwaka wa 2008 watu 400 wanauawa kila mwaka na polisi.

Polisi nchini Marekani wanaruhusiwa kutumia nguvu kulinda maisha yao wenyewe na ya wenzao.

Hata hivyo hakuna mbinu mwafaka ya kufuatilia kwa karibu matumizi ya risasi miongoni mwa polisi na iwapo mauaji yanatokea.

Kinaya ni kuwa serikali inawategemea maafisa hao hao wa polisi kuripoti iwapo wameua.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kulingana na takwimu hiyo watu weusi wamo katika hatari mara tatu zaidi ya kuuawa na polisi.

Ripoti hiyo ya maafisa 17,000 wa polisi mara nyingi haijumuishi visa vinavyosemekna kuwa vilitokea katika mazingira yasiyo na utata.

Washington Post imekuwa ikifuatilia kwa karibu vifo vyote vilivyotokea mikononi mwa polisi tangu kuanza kwa mwaka huu wakifanya mahojiano na kunukuu ripoti za polisi na zile za vyombo vya habari mashinani.

Gazeti hilo limegundua kuwa kunatokea takriban vifo2.6 kila siku ikilinganishwa na takwimu ya serikali ya kifo cha mtu mmoja 1.1 kila siku kwa mujibu wa takwimu za idara ya upelelezi ya FBI.

''Nataka kukueleza wazi kuwa vifo vilivyosababishwa na polisi haviripotiwi kamwe'' anasema aliyekuwa mkuu wa polisi Jim Bueermann.

''Hakuna njia yeyote ya kupunguza ama hata kukomesha mauaji ya kiholela ya watu iwapo hatutaanza kufuatilia na kuripoti visa hivi vya mauji ya polisi'' alisema Bueermann.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu 118 waliouawa walikuwa kati ya miaka 25-34,huku 94 wakiwa kati ya miaka 35-44.

Kulingana na takwimu hiyo watu weusi wamo katika hatari mara tatu zaidi ya kuuawa na polisi.

Asilimia kubwa ya watu weusi waliouawa walikuwa wamejihami ijapokuwa mmoja kati ya 6 hawakuwa wamejihami ama walikuwa wamebeba bastola bandia.

Wanaume 365 na wanawake 20 waliuawa na polisi

Watu 118 waliouawa walikuwa kati ya miaka 25-34,huku 94 wakiwa kati ya miaka 35-44.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanaume 365 na wanawake 20 waliuawa na polisi

8 kati ya wale waliouawa hawakuwa wamegonga miaka18

Visa vitatu pekee ndivyo vilivyofikishwa mahakamani.

Visa hivyo vilitokana na kuibuka video zilizoonesha polisi wakiwafukuza wahasiriwa na kisha kuwaua kwa risasi .