Kiongozi wa Georgia sasa ni gavana Ukraine

Haki miliki ya picha president.gov.ua
Image caption Kiongozi wa Georgia sasa ni gavana Ukraine

Rais wa Ukraine , Petro Poroshenko amemteua aliyekuwa kiongozi wa jamhuri ya Georgia, Mikheil Saakashivili, kuwa gavana wa jimbo lenye umuhimu mkubwa la Odessa.

Bwana Saakashvili, ambaye amekuwa akihudumu kama mshauri wa rais Poroshenko amepewa uraia wa Ukraine.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uteuzi wa bwana Saakashvili unatarajiwa kuudhi Moscow

Poroshenko alimmiminia sifa kochokocho bwana Saakashvili na kusema kuwa ni rafiki wa karibu wa watu wa Ukraine na hivyo alikuwa anamteua kuwa gavana.

Bwana Saakashvili sasa atawajibika kukabiliana na ushawishi mkubwa wa viongozi wa uliokuwa muungano wa kisovieti na matajiri waliosalia nchini Urusi.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa uteuzi huwa wa Bwana Saakashvili huenda ukawaudhi viongozi Urusi.

Haki miliki ya picha president.gov.ua
Image caption Serikali ya Poroshenko inapigana na uasi unaoungwa mkono na Urusi

Saakashvili anakumbukwa kwa sera zilizokuwazikiegemea upande wa Magharibi alipokuwa akiiongoza Georgia.

Aidha Bwana Saakashvili anakumbukwa kwa kuipeleka taifa lake japo dhaifu katika vita na jeshi la Urusi kuhusu jimbo dogo la kusini mwa Ossetia mwaka wa 2008.