Kim kardashian ni mjamzito

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kim kardashian

Nyota wa kipindi cha runinga nchini Marekani ambaye ameolewa na msanii kanye West amefichua siri katika kipindi cha keeping up with the Kardashians.

Kim Kardashian amefuchua kwamba amefanya ukaguzi wa damu na kubaini kwamba ni mjamzito.

''Nilifanya ukaguzi wa damu na nimegundua kwamba mimi ni mjamzito'',alimwambia dadaake Khloe Kardashian.

Kanda hiyo ya Video pia ilionyesha akienda kufanyiwa ukaguzi.

Huyu atakuwa mwamna wa pili wa nyota hao ambao walipata mtoto wao wa kwanza North West mwezi Juni mwaka 2013.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Kanye West na Kim Kardashian

Hakuna maelezo kuhusu ni lini mwana huyo atazaliwa.

Kabla ya kanda hiyo ya video kuonyeshwa ,Kim alituma ujumbe wake wa Twitter akisema kwamba ana habari njema za kutangaza.

Katika kipindi hicho Kim amekuwa akisema kwamba imekuwa vigumu kwa yeye na Kanye kupata mtoto mwengine.