Murray ajipa changamoto tenis

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Andy Murray akifurahi moja ya tuzo zake katika mchezo wa tenis

Mchezaji namba moja wa tenisi nchini Uingereza, Andy Murray amejipa changamoto ya kuongeza kiwango chake cha uchezaji wakati atakapopambana na Mfaransa Jeremy Chardy kuwania kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano ya French Open Jumatatu.

Mwingereza huyo nambari tatu kwa ubora duniani anapambana na mchezaji namba 45 kwa ubora.

Wachezaji hao wamekutana mara saba, kwa Murray kushinda mara sita ukiwemo mchezo wa uwanja wa udongo mjini Roma, Italia Mei 13.

Murray anaingia katika mchezo huo akiwa na rekodi ya kutofungwa michezo 13 mwaka huu.