Ban Ki-Moon alaani yanayojiri S Kusini

Image caption Mratibu wa maswala ya misaada ya kibinadamu , Toby Lanzer akitembelea kambi nchini Sudani kusini

Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa,Ban Ki-moon amelaani kufukuzwa kwa mratibu wa misaada ya kibinaadamu wa Umoja wa Mataifa bwana Toby Lanzer huko nchini Sudan Kusini . Ban ameitaka serikali hiyo kubadili uamuzi huo mara moja. Amesema Lanzer alikuwa mstari wa mbele katika kutafuta ufumbuzi mahitaji ya jamii iliyoathiriwa na mzozo wa nchi hiyo kwa kuhakikisha kwamba misaada inawafikia. Ban amesema swala hili ni muhimu sana hasa wakati huu wa vurugu zinazoendelea kwa pande zote mbili katika vita vya wenyewe kwa wenyewe,Vita hiyo ambayo imeua maelfu ya watu kuanzia Desemba mwaka 2013. awali, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alitoa wito pia kwa viongozi wa Sudan Kusini kumaliza mgogoro