Senate washindwa kuhuisha mkataba

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mkurugenzi wa CIA, John Brennan

Baraza la Senate la Marekani limeshindwa kuzuia kumalizika kwa muda wa saa mbili wa sheria ya kupambana na ugaidi ambapo Shirika la Usalama wa Taifa linakusanya kwa wingi taarifa katika simu za raia wa Marekani.

Katika mjadala wa Jumapili ambao ni nadra wajumbe wa Senate hawakukubali kuongezea muda wa kuendelea kwa sheria ya sasa ikiwepo migawanyiko miongoni mwa wajumbe wa chama cha Republican kwa kushindwa kuafikiana.

Baraza la Senate kwa sasa linajadili Muswada wa kuanzisha ufuatiliaji wa hatua za karibu zaidi.

Muswada ambao umekwisha pitishwa na Baraza la Wawakilishi.

Rais Obama na mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani,CIA, John Brennan, wameonya kuwa kushindwa kupitisha upya kwa hatua za ufuatiliaji vitendo vya kigaidi kutaifanya nchi kushindwa kufuatilia vitisho vya kigaidi.