Ajuza aokolewa katika boti iliozama China

Haki miliki ya picha XINHUA
Image caption Boti iliozama nchini China

Waokozi nchini Uchina wanaowasaka manusura kutoka kwenye meli ya abiria iliyozama katika mto Yangtze wameweza kumvuta kutoka kwenye meli hiyo mwanamke mwenye umri wa miaka 85.

Mwanamke huyo ni mmoja wa watu wapatao 12 wanaofahamika kunusurika katika ajali hiyo iliyotokea baada ya meli hiyo kuzama jana usiku .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Boti iliozama nchini China

Miili ya watu imekuwa ikivutwa kutoka kwenye meli hiyo.

Watu zaidi ya 450 walikuwa wameabiri meli hiyo ilipopata ajali kutokana na hali mbaya ya hewa.