Iraq yasema haisaidiwi kukabili IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Haider Al Abadi

Hatusaidiwi vya kutosha ,hayo ni maneno yake waziri mkuu wa Iraq ,Haider al-Abadi. Anasema kuna ushahidi mdogo sana wa kuwepo kwa uungwaji mkono wa kimataifa katika vita vyao dhidi ya wapiganaji wa Islamic State katika nchi yake Iraq.

Bw. Haider al-Abadi, ameonya kuwa kinyume na matarajio wanamgambo hao wa ISIS wanaendelea kuwasajili watu wengi kujiunga nao.

Matamshi hayo ya Bwana Abadi yanakuja wakati wa kikao kinachotarajia huko Ufaransa cha mataifa yaliyoungana kuipiga vita Islamic state.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa muungano nchini Iraq

Mawaziri wa maswala ya kigeni kutoka nchi hizo 20 wanakutana kujadili mikakati yao dhidi ya wanamgambo wa Islamic State walioko Iraq na Syria.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Paris anasema kuwa kutekwa kwa Ramadi na wapiganaji wa Islamic State kumeashiria kushindwa kwa mkakati uliopo sasa na kuongezeka kwa utegemezi wa Iraq kwa wanamgambo wa Shia wanaoungwa mkono na Iran .

Haki miliki ya picha AP
Image caption wapiganaji wa Islamic state

Waziri mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ni mmoja wa washiriki wa mazungumzo hayo .

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, amesitisha wizara yake baada ya kuvunjika mguu wake alipokua akiendesha baiskeli