Askari watoto wasajiliwa Islamic State

Image caption Watoto waliosajiliwa na wapiganaji wa Islamic State wakiswali

Picha za video katika simu ya mkononi ambazo BBC imezipata zinaonekana kuwaonyesha wapiganaji wa Islamic State wakimtesa mvulana wa Syria mwenye umri wa miaka 14.

Picha hiyo ambayo ilipigwa na mpiganaji aliyeasi kutoka kikundi hicho, inaonyesha mvulana huyo akipigwa wakati amefujngwa mikono yake.

Umoja wa Mataifa umeishutumu IS na makundi mengine yenye silaha nchini Syria na Iraq kwa kuwatesa na kuwaua watoto.

Watoto walisajiliwa, kufunzwa na kutumiwa katika uwanja wa vita.

Kijana mwingine ameiambia BBC namna alivyopigana na kuua kwa ajili ya kikundi cha al-Nusra Front chenye uhusiano na al-Qaeda. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15 tu na wakati huo alipojiunga na IS alimkuta kijana wa miaka 13 akifundishwa itikadi kali ya kidini.

Image caption Mvulana wa Syria akiadhibiwa na mpiganaji wa IS

Picha ya simu ya mkononi inamwonyesha Ahmed akiwa amening'inizwa mguu juu.

Amefungwa kitambaa usoni, na wanaume wawili wakiwa wameficha sura zao, wakiwa wamevaa nguo nyeusi kutoka juu hadi chini ya vidole vya miguu. Mmoja ana kifu na bastola na mwingine ana hangaika chumbani akiwana bunduki aina ya AK-47.

Ndani ya maeneo waliyojitangzia kuyatawala, Islamic State imeondoa mfumo wa elimu ya kawaida na badala yake kuanzisha shule za mtindo wa kijeshi ambazo zinawafundisha watoto iutikadi kali ya kidini na kuwafundisha kuua.

Islamic State wamekuwa wakiua nchini Syria na Iaraq, lakini madhara yake yataonekana zaidi baadaye.

Huu ni ufisadi wa karne. Watoto wa IS watakua kuwa watu wazima wakiwa wamefundishwa kuua na kujaa chuki na watazisumbua Syria na Iraq kwa miaka mingi ijayo.