Mlipuko wa bomu wawaua watu 20 Nigeria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko nchini Nigeria

Takriban watu 20 wamefariki kutokana na mlipuko wa bomu katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.

Mji huo ulikuwa umeshambuliwa saa za alfajiri siku ya jumanne na washukiwa wa kundi la Boko haram .

Saa chache baadaye ,mlipuaji wa kujitolea muhanga alijilipua katika soko la kuuza ngombe la Gamboru ndani ya mji huo kulingana na walioshuhudia.

Wakati wa kuapishwa kwake rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema kuwa anayahamisha makao makuu ya kijeshi katika vita dhidi ya wapiganaji hao kutoka mji mkuu wa Abuja hadi Maiduguri.