Idadi kubwa ya ndovu yatoweka Tanzania

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndovu

Wanaharakati wa wanyamapori wameelezea hali ya kutoweka kwa idadi ya ndovu kwa asilimia sitini nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kama janga.

Kundi linalofuatilia maisha ya wanyamapori, TRAFFIC, linasema idadi hiyo inaashiria kiwango halisi cha uwindaji haramu.

Waziri katika serikali ya Tanzania Lazaro Nyalandu, amesema kuwa tatizo hilo lipo kwa kiwango tofauti nchini humo, akitoa mfano kuwa eneo la Serengeti idadi yao inaongezeka .

Amesema mamia ya walinzi wa wanyamapori wamekodiwa kukabiliana na uwindaji haramu