Mwigizaji wa filamu ya Godzilla afariki

Image caption Godzilla

Hiroshi Koizumi ,msanii wa Japan ambaye aliigiza katika filamu nyingi za Godzilla amefariki akiwa na umri wa miaka 88.

Kulingana na ripoti,alifariki mjini Tokyo mnamo tarehe 31 Mwezi May kutokana na kichomi ama Pneumonia kwa kiingireza.

Koizumi aliigiza kama Godzilla katika filamu ya Godzilla Raids Again ikiwa ni falamu ya kwanza ya Godzilla iliozinduliwa mwaka uliofuta.

Baadaye aliigiza katika filamu kadhaa za kutisha ikiwemo Mothra,Godzilla vs The Thing na Ghindorah and the Three headed Monster.