Watakaowakamata magaidi kuzawadiwa Saudia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msikiti uliolipuliwa na mtu wa kujitolea muhanga

Utawala wa Saudia umetoa tangazo kwamba utatoa dola milioni mbili za Marekani kama zawadi kwa yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa wapiganaji wa kigaidi au kuzuia shambulio la kigaidi.

Ombi hilo limetolewa wakati utawala huo ulipokuwa ukiwataja washukiwa wa kisa cha milipuko ya waliojitolea mhanga iliofanyika katika misikiti miwili ya wa-Shia hapo mwezi jana.