Umoja wa Mataifa kuchunguza kashfa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameunda uchunguzi wa nje kuhusu kashfa ya kuwadhalilisha watoto kulikofanywa na wanajeshi wa Ufaransa wa kulinda amani nchini Jamahuri ya Afrika ya Kati.

Katika taarifa hiyo, Bwana Ban Ki Moon amesema Umoja wa Mataifa umedhamiria kuhakikisha kuwa hauwangushi waathirika wa vitendo hivi vya udhalilishaji, hasa vinapofanywa na watu wanaotegemewa kuwalinda.

Kuundwa kwa kamati huru ya uchunguzi ni moja ya madai ya wakosoaji ambao wamekuwa wakiukosoa Umoja wa Mataifa kwa kutochukua hatua madhubuti kuchunguza madai hayo ya udhalilishaji watoto wengine wakiwa na miaka tisa.Hatua hii imekuja mwaka mmoja kamili baada ya watafiti wa Umoja wa Mataifa kusikia kwanza kutoka kwa watoto walioathirika kutokana na udhalilishaji huo katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika Kati, Bangui.