Wapata chura ndani ya mkebe wa tomato

Image caption Chura chapatikana katika mkebe

Mtu na mkewe waliokuwa wakiandaa chakula cha mchana walipigwa na butwaa walipopata chura kilichokuwa kimekufa ndani ya mkebe wa tomato.

Muhammad na Sanam Hussain waligundua hayo wakati bi Hussain alipokuwa akipika mchuzi katika nyumba yao huko Alum Rock mjini Birmigham.

Bi Hussain ambaye ni mjamzito wa miezi saba amesema kuwa anaugua baada ya kukiona kiumbe hicho ndani ya mkebe wa tomato.

Kampuni ya Euro Foods inayouza bidhaa hiyo imesema kuwa inachunguza ni vipi chura hicho kiliingia ndani ya mkebe huo.

Image caption Chura chapatikana ndani ya mkebe wa tomato Uingereza

Bi Hussain amesema,''kwa kweli inachukiza ,nimeshtuka sana,nina wasiwasi kuhusu mtoto wangu kwa kuwa mimi ni mjamzito''.

''Nimeongea na mkunga wangu kuhusu niliyoyaona na akaniamibia niende hospitalini nitakaposikia vibaya.'',Mumewe amesema kuwa alishtushwa na makelele yaliopigwa na mkewe.

''Mke wangu alikuwa akiniandalia chakula cha mchana na mwanagun wa miezi 15 Wakati alipofungua mkebe huo alionekana na kuanza kupiga makelele akiniita''.