Uchina yakana udukuzi nchini Marekani

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Uhalifu wa mtandaoni

Uchina imetaja kama kukosa kuwajibika ipasavyo kwa Marekani kudai kuwa wadukuzi wa Uchina ndio waliosababisha udukuzi wa taarifa za ofisi za serikali ya Marekani.

Wizara ya mambo ya nje ya Uchina imesema ni vigumu kujua chanzo cha udukuzi huo na kwamba dhana isiyo na ushahidi wowote wa kisayansi haitasaidia.

Shirika la ujasusi la FBI chini Marekani linachunguza ni kwa namna gani wadukuzi wa komputa waliweza kuingilia taarifa hizo binafsi za wafanyakazi wa serikali wapatao milioni nne .

Ofisi ya utumishi ya nchini hiyo inasema karibu watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo.