Taarifa za wafanyakazi zadukuliwa US

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Barak Obama wa Marekani

Serikali ya marekani imekumbwa na udukuzi wa mtandao wa komputa ambapo taarifa binafsi za mamilioini ya wafanyakazi wa serikali zimeingiliwa.

Ofisi ya utumishi wa nchini inasema takriban watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udukuzi huo.

Idara ya Utumishi ya Serikali ya Marekani inayosimamisha huduma za wafanyakazi wa umma nchini huo imefanya uchunguzi wa usalama wa taarifa za wafanyakazi wake wapatao milioni nne.

Idara hiyo inasema wadukuzi hao walingilia taarifa hizo kwa njia ya mtandao tangu mwezi aprili jambo linalofanyiwa uchunguzi na shirika la kijasusi la FBI.

Taarifa zote za udukuzi huo na idadi ya watu waliohusika bado haijafahamika lakini afisa mmoja anasema kila idara ya serikali itakuwa imeathirika kwa kiasi kikubwa.

Mjumbe wa Kamati ya kiintelejensia ya baraza la Seneti imewalaumu wadukuzi kutoka nchini China kwa kuhusika na udukuzi huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa taarifa muhimu kama kama hizo kufanyiwa udukuzi.

Mwezi Machi mwaka jana,wadukuzi walijaribu kuwadukua wafanyakazi wa serikalini ambapo pia mwezi Novemba taarifa za wafanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani wapatao elfu ishirini zilidakuliwa.