Watu 400 wafariki katika mto Yangtse

Haki miliki ya picha AP
Image caption Meli iliozama katika mto Yangtse nchini China

Msemaji wa serikali nchini China anasema kuwa karibu watu 400 wanahofiwa kuaga dunia wakati feri ilipozama kwenye mto Yangtze siku ya jumatatu.

Idadi hiyo imeongezeka kwa haraka baada ya makundi ya uokoaji kusaka vyumba vya feri hiyo.

Kwa sasa meli hiyo imendolewa majini kwa kutumia mitambo mikubwa.

Jumla ya watu 456 walikuwa ndani ya feri hiyo wakati ilipokumbwa na dhoruba ambapo ni watu 14 tu walioripotiwa kuponea ajali hiyo.

Ajali hiyo inaripotiwa kuwa mbaya zaidi nchini humo tangu miaka 60 iliyopita.