Houthi washambulia Saudi Arabia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mpiganaji wa Houthi

Saudi Arabia inasema kuwa imezuia makombora yaliyofyatuliwa kutoka nchini Yemen kwenda ardhi yake na waasi wa Houthi.

Utawala unasema kuwa makombora hayo yalikuwa yamelenga mji wa Khamees Mushait mapema leo lakini yakadunguliwa .

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waasi wa Houthi

Mashambulizi hayo yalifanyika baada ya Saudi Arabia kuripoti mapigano yaliyodumu saa kadha siku ya Ijumaa maeneo ya mpaka ya Jizan na Najran.

Shirika moja la habari lilisema kuwa raia wanne wa Saudi Arabia waliuawa na watu wengine kadha nchini Yemen wakati jeshi lilipopambana na waasi wa Houthi watiifu kwa rais wa zamani ya Yemen Ali Abdullah Saleh.

Wakazi wa mji mkuu Sanaa wanasema kuwa mji huo baadaye ulishambuliwa vikali na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.