Barua yasema Mbeki na Blatter walikubaliana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Blatter

Barua pepe iliopatikana na gazeti moja la Afrika kusini na kuonekana na BBC inatoa ushahidi zaidi kwamba aliyekuwa rais wa taifa hilo Thabo Mbeki na rais wa FIFA Sepp Blatter walikubaliana kuhusu kitita cha dola millioni kumi ambacho maafisa wa mashtaka nchini Marekani wanasema ilikuwa hongo ya taifa la Afrika Kusini kupewa maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2010.

Katika barua hiyo katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke alimuandikia waziri mmoja wa Afrika Kusini akimtaka kueleza ni lini fedha hizo zitatolewa kwa kuwa tayari Blatter na Mbeki walijadiliana kuhusu swala hilo.

Serikali ya Afrika Kusini inasisitiza kuwa fedha hizo zilitolewa kihalali kukuza soka katika visiwa vya Carebbean.