Dola milioni 10 za FIFA zililipwa Warner

Image caption Shirikisho la kandanda duniani FIFA

Uchunguzi wa BBC umegundua jinsi zilivyotumika kiasi cha dola milioni 10 zilizotumwa kutoka FIFA kwenda kwa akaunti za aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner.

Pesa hizo zilipangiwa kutumiwa na shirika moja la Afrika Kusini katika nchi za Caribbean.

Lakini nyaraka ambazo zilikaguliwa na BBC zinasema kuwa bwana Warner alitumia pesa hizo kwa mikopo yake ya kibinafsi na kwa ulanguzi wa pesa.

Haki miliki ya picha none
Image caption Makamu wa rais wa zamani wa FIFA Jack Warner

Karibu nusu ya pesa hizo zililipwa kwa maduka ya jumla nchini Trinidad ambapo ni nyumbani kwao Warner.

Waendesha mashtaka nchini Marekani wanasema kuwa kisha mpesa hizo zilirudishwa kwake katika sarafu ya nchi hiyo huku karibu dola laki tatu zikitolewa kwa benki na watu wenye uhusiano wa karibu naye.

Malipo hayo yanafanyiwa uchunguzi na shirika la ujasusi la Marekani FBI na ni moja ya kashfa zinazolikumba shirikisho la kandanda duniani FIFA.