Nchi za G7 zandaa mkutano Ujerumani

Haki miliki ya picha PA
Image caption Viongozi wa nchi za G7

Ujerumani inandaaa mkutano wa kundi la nchi zilizostawi kiviwanda duniani za G7 kwa muda siku mbili zinazokuja. Mkutano huo unatarajiwa kutawaliwa na suala la mzozo uliopo mashariki mwa ukrain pamoja na suala na deni la ugiriki.

Mwandishi wa BBC mjini Bavaria anasema kuwa ujerumani inataka mkutano huo kukubaliana kuhusu hatua za pamoja za kuzuia nchi yoyote kuacha kuunga mkono vikwazo ambavyo vimeathiri uchumi wa urusi.

Chansela wa ujerumani Angela Merkel pia atatangaza mipango yake ya kutaka kufanyiwa mabadiliko hatua za kimataifa za kukabiliana na majanga kama ebola, na njia za kuzisaidia nchi zinazoendela kuweza kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.