Uchaguzi wa ubunge wafanyika Uturuki

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Mpiga kura nchini Uturuki

Uturuki inandaa uchaguzi wake wa ubunge leo jumapili. Matokeo ya kura hiyo yataamua ikiwa chama tawala cha AK cha rais Recep Tayyip Erdogan kitapa ushindi wa kukiwezesha kuifanyiamabadiliko katiba na kuifanya Uturuki kuwa nchi inayongozwa na rais.

AK kimeshinda kila uchaguzi tangu mwaka 2012 lakini bwana Erdogan amekuwa akilaumiwa kufuatia uongozi wake unaofananishwa na wa kiimla.

Ikiwa chama cha HDP kitapata zaidi ya asilimia 10 na kuingia bungeni kwa mara ya kwanza kitainyima serikali theluthi mbili ya viti inavyohitaji.