Raia wa Uturuki wanapiga kura ya ubunge

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Uturuki

Uturuki inandaa uchaguzi wake wa ubunge leo jumapili.

Matokeo ya kura hiyo yataamua iwapo chama tawala cha AK cha rais Recep Tayyip Erdogan kitapata ushindi wa kukiwezesha kuifanyia katiba mabadiliko na kuifanya Uturuki kuwa nchi inayoongozwa na rais.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wa Uturuki washiriki katika uchaguzi wa ubunge

AK kimeshinda kila uchaguzi tangu mwaka 2012 lakini bwana Erdogan amekuwa akilaumiwa kufuatia uongozi wake unaofanana na wa kiimla.

Ikiwa chama cha HDP kitapata zaidi ya asilimia 10 na kuingia bungeni kwa mara ya kwanza kitainyima serikali theluthi mbili ya viti inavyohitaji.