Mashirika ya ndege kushtakiwa Uingereza

Image caption Mashirika ya ndege kushtakiwa Uingereza

Wahudumu 17 wa zamani na wa sasa wa ndege wanapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mashirika ya ndege chini Uingereza, wakisema kuwa wameathiriwa kiafya na hewa chafu ndani ya vyumba vya ndege.

Kesi hiyo inagharamiwa na chama ambacho kinawawakilisha karibu wahudumu wa ndege 20,000.

Wafanyikazi hao wanaamini kuwa wamekuwa wagonjwa baada ya kupumua moshi uliochanganya na mafuta ya injini na chemical zingine chafu.

Chama hicho cha Unite union ambacho kinataka kufanyika uchunguzi kuhusu kuchafuka kwa hewa ndani ya vyumba vya wahumudmu wa ndege, juzi kimefungua kitengo cha kurekedi na kushughulikia malalamiko kutoka kwa wanachama wake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashirika ya ndege kushtakiwa Uingereza

Ripoti zilizowasilishwa kwa halmashuri ya safari za ndege zinaonyesha kuwa kati ya Aprili mwaka 2014 na Mei mwaka 2015 visa tofauti vya moshi ndani ya ndege kubwa za abiria viliripotiwa kwenye ndege zinazomilikiwa na shirika la ndege la Uingereza.

Pia kuna ripoti ya rubani mmoja anayefanya kazi na shirika moja kuu la Uingereza ambaye anaamini kuwa aliathiriwa na moshi chafu alipokuwa akitua katika uwanja wa Birmingham mwaka 2014.