Mguu bandia wenye hisia wazinduliwa

Image caption Mguu bandia wenye hisia wazinduliwa

Watafiti katika chuo kikuu nchini Ausralia wamevumbua mguu wa kwanza bandia duniani wenye uwezo wa kusisimua hisia halisi za binadamu.

Mguu huo wenye tofauti chache mno na ule halisi unahisi hata maumizi.

Katika uvumbuzi huo wa Profesa Hubert Egger wa chuo kikuu cha Upper Austria, mguu huo bandia unatumia neva za mwili wa mtu aliyekatwa mguu wake.

Image caption Watafiti katika chuo kikuu nchini Austria wamevumbua mguu bandia wa kwanza duniani wenye hisia halisi za binadamu.

Aidha neva za ncha za mguu wa mgonjwa hushikanishwa na waya zinazowasiliana na ubongo kupitia kwa paja.

Professor Egger anaelezea kuwa bwana mmoja mlemavu amekuwa akiuvaa mguu huo bandia kwa miezi sita.

Image caption Bwana Wolfgang Rangger amekuwa na mguu huo bandia kwa miezi sita

Bwana Wolfgang Rangger alisema kuwa katika muda huo wa miezi sita anauwezo wa kubaini iwapo anakanyaga mawe, simiti,na hata nyasi.

''ninapo kanyaga jiwe,nahisi kitu kigumu na pia nikikanyaga mbao,pia najua kuwa kile nilichokanyaga ni tofauti.''

''Nimepata maisha mapya baada ya kupokea mguu bandia'' alisema Wolfgang Rangger.