China yatetea haki zake za binadamu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption China yatetea haki zake za binadamu

Serikali ya China imesifu jitihada zake za kulinda haki za binadamu za watu wake wakati ambapo waangalizi wengi wanasema kuwa kuna vizingiti vingi kwa haki hizo.

Kwenye ripoti ya kurasa 14,000, China inasema kuwa inalinda haki za watu za demokrasia, hukumu zisizokuwa zenye haki na mazingira masafi.

Lakini mashirika ya haki za binadamu yanasema kuwa chini ya uongozi wa rais Xi Jinping, China imeweka vizuizi vikubwa katika maisha ya watu hasa vyuo vikuu, mitandao, vyombo vya habari na mashirika yasiyokuwa ya serikali.

Wale wanaoikashifu serikali nchini China mara nyingi hufungwa.