Mtandao wa kijeshi Marekani wadukuliwa

Haki miliki ya picha
Image caption Mkuu wa viongozi wa kijeshi nchini Marekani akiwa na waziri wake wa ulinzi Ash Carter

Jeshi la Marekani lilisimamisha kwa muda mtandao wake baada ya kisa cha kuingiliwa kimitandao. Jeshi la Syria la Electroniki - linalomuunga mkono Rais Bashar al-Assad - limesema katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, kuwa ndilo lililotekeleza shambulizi hilo la kimitandao. Lakini habari za hivi punde zasema kuwa mtandao huo wa jeshi la Marekani umerejeshwa.