Raia 20 wauawa Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia 20 wauawa Syria

Ripoti kutoka nchini Syria zinasema kuwa takriban watu 20 wameuawa kufuatia mashambulizi ya angani yaliyoendeshwa na serikali kwenye mji ulio kaskazini mwa nchi.

Kulingana na shirika moja la haki za binadamu lenye makao yake nchini Uingereza, ni kuwa watoto kadha ni miongoni mwa wale waliouawa wakati lilipofanywa shambulizi eneo linalodhibitiwa na waasi katika mji wa Al-Janudiyah.

Mji huo uko kwenye mkoa wa Idlib ambapo serikali imekuwa ikipoteza ngome zake siku za hivi majuzi.