Urusi yapingwa dhidi ya Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mjadala kuhusiana na Urusi kuishambulia Ukraine waendelea

Viongozi wa kundi la G7 kutoka nchi tajiri za viwanda wamefungua mkutano wao wa mwaka huko nchini Ujerumani kusini huku wakipinga vitendo vya Urusi kwa nchi ya Ukraine.

Rais Barack Obama wa Marekani na Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani kwa pamoja wamesisitiza kwamba Urusi inapaswa kuheshimu vipengele vya makubaliano yaliyofikiwa huko Minsk kwa kuitaka nchi hiyo kuheshimu utawala wa Ukraine.

Urusi yenyewe imetengwa katika mkutano huo. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kuwa ana imani wanachama wa umoja wa Ulaya watakubali kurefusha vikwazo dhidi ya Moscow ambavyo vinaisha muda wake mwezi July mwaka huu.

Akizungumza na BBC, Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond, ameunga mkono kuendelezwa kwa vikwazo dhidi ya Urusi kutokana na vitendo vyake dhidi ya Ukraine.

Kuendeleza vikwazo hivi ni alama kubwa ambayo twaweza kuituma kwa Urusi ya kwamba nchi za Magharibi zitasimama pamoja, huku Ulaya, Marekani na nchi zingine, zinataka maridhiano kamili na wajibu ya kuwa Urusi imeingia katika makubaliano ya Minsk." amesema PHILI HAMMOND

Hammond ameonya kuwa kama nchi za Magharibi zingezidisha vikwazo vyake, iwapo hali nchini Ukraine ingezidi kuwa mbaya." Kama mapigano yanaendelea na kuna ukiukwaji zaidi wa kusimamisha mapigano, kwa mfano kulikuwa na mashambulio ya Urusi kwenye bandari ya Mariupol kitu ambacho watu wamekuwa wakikichunguza, kisha EU imekuwa ikifahamu: tutazidisha vikwazo na maafisa wa EU tayari wamekuwa wakipewa kazi kuandaa chaguo kwa ajili ya vikwazo zaidi kama kulikuwa na kuenea zaidi kwa chuki."

Kwa upande wake, rais Obama amesema kuwa viongozi wa G7 watajadili namna ya kusimamia kile alichokiita chokochoko za Urusi kwa Ukraine.Akizungumza katika sherehe za ufunguzi zilizoandaliwa kwaajili yake, Obama aliainisha ajenda za mkutano huo.

"tunaenda kujadili mipango yetu ya baadae, uchumi wa dunia ambao unatengeneza nafasi za ajira, kudumisha nguvu na mafanikio ya muungano wetu, kutengeneza ushirikiano mpya wa kibiashara katika ukanda wa Atlantic, kusimamia chokochoko za Urusi dhidi ya Ukrane,kupambana na vitisho vya mabadiliko ya tabia ya nchi."