Bangladesh:ndoa za mapema zimeenea sana

Haki miliki ya picha
Image caption UNHCR yashauri Bangladesh ipige vita ndoa za mapema

Shirika la kutetea haki za kibinadamu, Human Rights Watch,limetoa wito kwa serikali ya Bangladesh itekeleze ahadi yake ya kukabiliana na visa vingi vya ndoa za mapema nchini humo.

Aidha Shirika hilo limeiomba serikali hiyo kuachana na mpango wake wa kupunguza umri ambao msichana ataruhusiwa kuolewa kutoka miaka 18 hadi 16.

Takriban asilimia 30 ya mabibi harusi nchini Bangladesh huwa chini ya umri wa miaka 15 licha ya kuwa hairuhusiwi kisheria.

Image caption Bangladesh:ndoa za mapema zimeenea sana

Viwango vya juu vya umaskini vimelaumiwa kuwashinikiza wazazi wengi kuwaoza watoto wao wakike wakiwa bado wachanga.

Wazazi hao huwaoza kwa dhana kuwa huwenda wakapata maisha bora ndani ya ndoa lakini badala yake, wengi hukabiliwa na matatizo zaidi yanayojiri hasa ya kiafya ,kielimu, kiuchumi na kijamii.