Warner afanyiwa uchunguzi zaidi

Haki miliki ya picha Warner TV
Image caption Warner afanyiwa uchunguzi zaidi

Uchunguzi unaendelea kuhusu masuala ya kifedha ya aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho la kandanda dunia FIFA Jack Warner.

Pesa zilizolipwa na shirikisho la kandanda la Australia ili iweze kushinda fursa ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2022 zinadaiwa kuelekezwa kwa akaunti ya Warner

Image caption Warner afanyiwa uchunguzi zaidi

Frank Lowy, ambaye aliongoza jitihada za Australia za kupigania fursa ya kuandaa kombe la dunia, alisema kuwa malipo hayo yalinuiwa kuboresha mchezo wa kandanda nchini Trinidad and Tobago na hivyo hazikuwa hongo.

Siku ya Jumatatu BBC ilifahamu kuwa bwana Warner alikuwa alichunguzwa kutokana na kutoweka kwa pesa zilizotolewa kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Haiti. Hata hivyo amekana madai hayo.